Jun 16, 2018 16:09 UTC
  • HAMAS yamuomba msaada Sayyid Hassan Nasrullah kuhusu wakimbizi wa Palestina

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), Ismail Haniya amemtumia ujumbe Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, akimuomba msaada kwa ajili ya kutatuliwa matatizo ya wakimbizi wa Kipalestina hususan wale walioko katika kambi ya wakimbizi ya Ain al-Hilweh.

Katika ujumbe huo Haniya ameeleza mapenzi waliyonayo wakimbizi wa Palestina kwa taifa la Lebanon na amemuomba kiongozi wa Hizbullah achukue hatua madhubuti kwa ajili ya kutatuliwa matatizo yanayowakabili wakimbizi hao katika kambi ya Ain al-Hilweh.

Ismail Haniya anasisitzia kuwa, kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kuweka milango ya umeme katika maeneo ya kuingilia kwenye kambi hiyo kutasaidia kuimarisha usalama kwa wakazi wa kambi hiyo.

Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyidi Hassan Nasrullah

Kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Ain al-Hilweh ndiyo kubwa zaidi ya wakimbizi wa palestina huko karibu na mji wa Sidon, kusini mwa Lebanon na inahifadhi maelfu ya wakimbizi wa Palestina kwa miaka mingi.

Kwa mujibu wa makubaliano ya makundi ya Kipalestina na serikali ya Lebanon, jukumu la kulinda usalama wa kambi hiyo liko mikononi mwa makundi ya Kipalestina. Hadi sasa kambi hiyo imeshuhudia mapigano kadhaa kati ya makundi ya Kipalestina na magaidi wa Kiwahabi waliotaka kuidhibiti kambi hiyo kwa ajili ya kuendeshea harakati zao za kigaidi.

Tags