Daesh yaua makumi kwa gesi ya sumu huko Sheikh Maqsood
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4636-daesh_yaua_makumi_kwa_gesi_ya_sumu_huko_sheikh_maqsood
Watu wasiopungua 23 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika shambulio la silaha za kemikali lililofanywa na magaidi wa kundi la Daesh dhidi ya wapiganaji a Kikurdi wa People's Protection Units (YPG) karibu na mji wa Aleppo nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 08, 2016 04:46 UTC
  • Daesh yaua makumi kwa gesi ya sumu huko Sheikh Maqsood

Watu wasiopungua 23 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika shambulio la silaha za kemikali lililofanywa na magaidi wa kundi la Daesh dhidi ya wapiganaji a Kikurdi wa People's Protection Units (YPG) karibu na mji wa Aleppo nchini Syria.

Shambulizi hilo lilifanyika jioni ya jana na kusababisha fazaa kubwa miongoni mwa mwakazi wa eneo Sheikh Maqsood lililoko umbali wa kilomita 355 kutoka mji mkuu wa Syria, Damascus. Habari ya shambulizi hilo la silaha za sumu pia imethibitishwa na Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Wakurdi ya Heyva Sor.

Madaktari wa eneo la Sheikh Maqsood wanasema wamepokea majeruhi wengi walioathiriwa na silaha za kemikali.

Hayo yamekuja siku tatu baada ya televisheni ya al-Ikhbariyah ya Syria kutangaza kuwa magaidi wa Daesh wamelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa mji wa mashariki wa Dayr al-Zawr kwa kutumia makombora yenye gesi ya haradali.

Agosti mwaka 2013 mamia ya watu waliuawa katika shambulizi la silaha za kemikali la magaidi wa Daesh lililolenga kitongoji cha Ghouta huko Damascus.