Jul 31, 2018 14:32 UTC
  • UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Saudia

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa kuendelea kukamatwa wapinzani wa serikali nchini Saudi Arabia.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa, marekebisho yaliyofanyika nchini Saudi Arabia yamepuuza haki za kiraia na za kisiasa. 

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuachiwa haraka wanaharakati wa masuala ya kijamii na kuwataka maafisa wa serikali ya Riyadh kuwaachia huru wanawake waliofungwa jela kwa sababu ya kupinga sheria ya kupiga marufuku wanawake kuendesha magari. 

Awali Norway ilikuwa tayari imekosoa vikali hali mbaya ya haki za binadamu nchini Saudi Arabia. 

Maaelfu ya wanaharakati wanashikiliwa katika jela za Saudi Arabia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Ine Marie Eriksen Soreide amekosoa vikali kesi za kunyongwa watu, kufungwa jela watetezi wa haki za binadamu na kubinywa uhuru wa kujieleza na kusema nchini Saudi Arabia na kusema, marekebisho yaliyofanyika nchini humo ni ya kimaonyesho tu. 

Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman anaendelea kupingwa vikali ndani na nje ya nchi hiyo kutokana na sera zake za kuwakandamiza na kuwafuta wapinzani na wanaharakati wa kisiasa na wa masuala ya haki za binadamu nchini humo. 

Tags