Australia yafuata mkumbo, yaitambua Quds kuwa mji mkuu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50180-australia_yafuata_mkumbo_yaitambua_quds_kuwa_mji_mkuu_wa_israel
Australia imesema inautambua mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
(last modified 2026-02-17T02:26:49+00:00 )
Dec 15, 2018 06:53 UTC
  • Australia yafuata mkumbo, yaitambua Quds kuwa mji mkuu wa Israel

Australia imesema inautambua mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.

Waziri Mkuu wa Autralia, Scott Morrison ametoa tangazo hilo leo Jumamosi kutoka mji mkuu Sydney na kuongeza kuwa, "Australia sasa inatambua magharibi mwa Quds ambayo ni makao makuu ya Bunge la Israel (Knesset) na taasisi nyingi za serikali, kama mji mkuu wa Israel."

Amesema, "Australia sasa imelitambua rasmi eneo la magharibi mwa Quds ambayo ni makao makuu ya Bunge la Israel (Knesset) na taasisi nyingine za serikali kuwa mji mkuu wa Israel. Tutafungua ofisi za ulinzi na biashara katika mji huo, lakini tutauhamishia ubalozi wetu mjini hapo kutoka Tel Aviv baada ya kukamilishia masuala ya msingi."

Uzinduzi wa ubalozi wa Marekani Quds

Hayo yanajiri siku chache baada ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuitahadharisha Brazil dhidi ya mpango wake wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds kutoka Tel Aviv, zikisisitiza kwamba hatua hiyo itakuwa na athari mbaya katika uhusiano wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini na nchi za Kiarabu.

Rais wa Marekani tarehe 6 Disemba mwaka jana 2017 alitangaza Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel; na Mei 14 mwaka huu Washington ikauhamishia ubalozi wake katika mji huo wa Waislamu kutoka Tel Aviv.

Tayari Guatemala imefuata kibubusa mkumbo huo wa Marekani wa kuuhamishia ubalozi wake mjini Quds kutoka Tel Aviv.