Lavrov: Mashambulizi ya anga Syria yataendelea hadi kushindwa kikamilifu magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i535-lavrov_mashambulizi_ya_anga_syria_yataendelea_hadi_kushindwa_kikamilifu_magaidi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa Moscow itaendeleza mashambulizi yake ya anga huko Syria hadi pale makundi ya kigaidi yatakaposhindwa kikamilifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2016 23:58 UTC
  • Lavrov: Mashambulizi ya anga Syria yataendelea hadi kushindwa kikamilifu magaidi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa Moscow itaendeleza mashambulizi yake ya anga huko Syria hadi pale makundi ya kigaidi yatakaposhindwa kikamilifu.

Sergei Lavrov ambaye yuko ziarani nchini Oman amesema kuwa mashambulizi ya anga ya nchi hiyo hayatasita hadi pale makundi ya kigaidi kama Daesh na Jabatul Nusra yatakapopata pigo kikamifu. Lavrov amesema, haoni sababu ya nchi yake kusitisha mashambulizi hayo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa moja ya masharti ya kusimamishwa mashambulizi ya anga ya nchi yake huko Syria ni kusitishwa harakati za magendo kati ya Syria na Uturuki.

Russia inamtuhumu Rais Recep Tayyip Erdgan wa Uturuki na familia yake kwa kuliunga mkono kundi la kigaidi la Daesh kupitia biashara haramu ya mafuta, madai ambayo yamekanushwa na Ankara.