Wasiwasi wa Daesh kupata silaha za kemikali
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i5797-wasiwasi_wa_daesh_kupata_silaha_za_kemikali
Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) imetahadharisha kwamba kuna uwezekano kundi la kigaidi la Daesh likawa na silaha za kemikali.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 26, 2016 02:35 UTC
  • Wasiwasi wa Daesh kupata silaha za kemikali

Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) imetahadharisha kwamba kuna uwezekano kundi la kigaidi la Daesh likawa na silaha za kemikali.

Jumuiya hiyo imetangaza kuwa, kuenea habari za kugongana zinazosema kuwa kundi la Daesh lina silaha hatari kama za kemikali kunatia wasiwasi mkubwa. Taarifa hiyo imesema jumuiya ya OPCW itadumisha juhudi za kuhakikisha kundi hilo halipati na kutumia silaha za aina hiyo.

Taarifa hiyo ya Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) imetolewa kufuatia habari ya makundi ya kulinda Wakurdi wa Syria na jumuiya ya kusimamia haki za binadamu huko Syria kutangaza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh lilitumia gesi ya sumu katika mashambulizi yake ya mwezi Juni mwaka jana dhidi ya maeneo yamayodhibitiwa na Wakurdi huko kaskazini mwa Syria.

Kundi hilo la kigaidi linalodhibiti baadhi ya maeneo ya Syria limetumia silaha za kemikali mara kadhaa dhidi ya raia na kufanya jinai za kutisha.