Imarati kufungua ubalozi wake Israel ndani ya miezi 5
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63241-imarati_kufungua_ubalozi_wake_israel_ndani_ya_miezi_5
Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema nchi hiyo inatazamiwa kufungua ubalozi ndani ya utawala haramu wa Israel katika kipindi cha kati ya miezi mitatu hadi mitano.
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Sep 05, 2020 06:53 UTC
  • Imarati kufungua ubalozi wake Israel ndani ya miezi 5

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema nchi hiyo inatazamiwa kufungua ubalozi ndani ya utawala haramu wa Israel katika kipindi cha kati ya miezi mitatu hadi mitano.

Gazeti la Hayom la utawala wa Kizayuni limemnukuu afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwa wa Wizara ya Mambo ye Nchi za Nje ya Imarati akisema hayo na kuongeza kuwa, baada ya kufunguliwa ubalozi huo, Waisraeli wataanza kuitembelea nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi bila kizingiti chochote.

Afisa huyo wa Imarati amefichua kuwa, UAE inatafakari juu ya suala la kufungua pia ubalozi mdogo ama katika mji wa Haifa au Nazareth ili kuwepesisha shughuli hizo za kibalozi baina ya tawala mbili hizo.

Mapema wiki hii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilisema utawala huo pamoja na maafisa wa Umoja wa Falme za Kiarabu wakishirikiana na maafisa wa Marekani, wameshajadili na kuafikiana juu ya suala hilo la kufunguliwa ofisi za kibalozi.

Waislamu duniani wamesema hatua ya UAE ni sawa na kuwapiga jambia kwa nyuma

Agosti 31, kwa mara ya kwanza ndege ya moja kwa moja ya utawala haramu wa Israel ilitua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Abu Dhabi ikiwa na wajumbe wa Tel Aviv na Washington, wiki mbili baada ya Imarati na utawala huo wa Kizayuni kusaini mkataba na kuafikiana rasmi kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Makubaliano hayo yamekabiliwa na wimbi kali la malalamiko na upinzani wa makundi ya Palestina, nchi za Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi na shakhsia kadhaa wa kisiasa, kijamii na kidini kote duniani.