Shirika la ndege la Bahrain latiliana saini mikataba mitano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65121-shirika_la_ndege_la_bahrain_latiliana_saini_mikataba_mitano_na_israel
Shirika la ndege la ukoo wa kifalme wa Aal Khalifa nchini Bahrain, umetia saini mikataba mitano na mashirika na taasisi mbalimbali za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao mikono yake imejaa damu za wananchi madhlumu wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2020 23:25 UTC
  • Shirika la ndege la Bahrain latiliana saini mikataba mitano na Israel

Shirika la ndege la ukoo wa kifalme wa Aal Khalifa nchini Bahrain, umetia saini mikataba mitano na mashirika na taasisi mbalimbali za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao mikono yake imejaa damu za wananchi madhlumu wa Palestina.

Mtandao wa habari wa "al Arabi 21" umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, katika ziara ya ujumbe wa kiuchumi wa Bahrain wa kutembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel, shirika la ndege la Bahrain liitwalo "Tayaran al Khaleej" au "Gulf Air" limetiliana saini mikataba mitano na taasisi na mashirika mbalimbali ya utawala wa Kizayuni.

Wiki mbili zilizopita pia, ujumbe mmoja wa Bahrain ulitia saini hati tatu za maelewano na hoteli ya Kizayuni ya Waldorf Astoria katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Gulf Air (Tayaran al Khaleej)

 

Vile vile ujumbe huo wa Bahrain ulitiliana saini na mashirika ya Kizayuni mikataba mbalimbali ya teknolojia, ubunifu, na mazingira. Mikataba hiyo ilitiwa saini baina ya serikali ya kiimla ya Bahrain na mashirika madogo madogo na ya kati na kati ya utawala wa Kizayuni.

Mwezi Septemba mwaka huu, Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel zilitiliana saini makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida baina yao ikiwa ni kutangaza rasmi uhusiano wa pande hizo mbili uliokuwepo kwa miaka mingi baina yao kwa njia za siri.