Oman: Hatuna haraka ya kupanua uhusiano wetu na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66792-oman_hatuna_haraka_ya_kupanua_uhusiano_wetu_na_israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema, nchi yake haina haraka ya kupanua uhusiano wake na Israel na wala haikusudii kuchukua hatua ya kufanya hivyo kwa sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2021 23:27 UTC
  • Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Al Busaidi
    Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Al Busaidi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema, nchi yake haina haraka ya kupanua uhusiano wake na Israel na wala haikusudii kuchukua hatua ya kufanya hivyo kwa sasa.

Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Al Busaidi ameeleza kwamba, kinyume na majirani zake wa Kiarabu, Muscat haitaharakisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha AlBusaid amedai kwamba, Oman ingali inafungamana na msimamo wa kuundwa nchi huru ya Palestina, kwa sababu bila kuhitimishwa ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina, amani jumuishi na ya kiuadilifu baina ya nchi za Kiarabu na Israel haitapatikana.

 

Aliyekuwa mfalme wa Oman hayati Sultan Qaboos (kulia) alipomkaribisha waziri mkuu wa Israel Netanyahu mjini Muscat kwa mazungumzo

Kwa mashinikizo ya Marekani, hadi sasa nchi nne za Kiarabu za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocoo zimeafiki kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Oman haina uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni  wa Israel, lakini pamoja na hayo, hadi sasa viongozi wa pande hizo mbili wameshakutana mara kadhaa na kufanya mazungumzo.../