Palestina yataka kuharakishwa kufuatiliwa jinai za kivita za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66872-palestina_yataka_kuharakishwa_kufuatiliwa_jinai_za_kivita_za_israel
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina jana usiku ilitoa tamko na kutaka kuharakishwa kufuatiliwa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2021 04:21 UTC
  • Palestina yataka kuharakishwa kufuatiliwa jinai za kivita za Israel

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina jana usiku ilitoa tamko na kutaka kuharakishwa kufuatiliwa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Shirika la habari la WAFA la Palestina limeinukuu wizara hiyo ikisema katika taarifa yake kwamba, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao makuu yake huko The Hague Uholanzi inapaswa kuanzisha uchunguzi wa harakati kuhusu jinai za Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina.

Vile vile Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imetaka kuadhibiwa kila aliyetenda jinai dhidi ya haki ya wananchi wa Palestina.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina pia imelaani katika tamko hilo jinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwakandamiza wananchi wa Palestina na matukufu yao likiwa ni moja ya malengo ya upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi wanazoporwa Wapalestina.

Wazayuni wanafanya jinai kubwa hata kwa watoto wadogo wa Palestina

 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina vile vile imeitaka jamii ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu na ya misaada ya kibinadamu kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel uheshimu sheria za kimataifa na ihakikishe kunatolea adhabu haraka kwa Wazayuni waliotenda jinai dhidi ya Wapalestina.

Tarehe 5 mwezi huu wa Februari 2021, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hukumu ya kuthibitisha kwamba ina nguvu za kisheria za kufuatilia jinai zilizofanywa na Wazayuni mwaka 1967 dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa, ardhi ya Palestina inajumuisha ardhi zote zilizotekwa na Wazayuni mwaka 1967.