Lebanon yalaani madai ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68004-lebanon_yalaani_madai_ya_utawala_wa_kizayuni_wa_israel_kuhusu_hizbullah
Balozi wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa amelaani madai yaliyotolewa hivi karibuni na viongozi wa Kizayuni dhidi ya Hizbullah akisisitiza kuwa hayana msingi na yanaingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2021 23:18 UTC
  • Lebanon yalaani madai ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Hizbullah

Balozi wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa amelaani madai yaliyotolewa hivi karibuni na viongozi wa Kizayuni dhidi ya Hizbullah akisisitiza kuwa hayana msingi na yanaingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Salim Baddoura amesema: "kwa mtazamo wetu sisi, hotuba aliyotoa mwakilishi wa Israel ya kuituhumu Hizbullah kuwa ni harakati ya kigaidi na kwamba mtambo wa makombora ya ulinzi wa muqawama wa Kiislamu ni tishio dhidi ya Walebanon, ni ya kutupiliwa mbali na haikubaliki."

Mnamo mwezi Januari mwaka huu pia, balozi wa Lebanon katika UN alijibu matamshi ya uongo aliyotoa mwakilishi wa Israel katika umoja huo na akasisitiza kuwa, Hizbullah ni kikosi cha Lebanon kinachowakilisha idadi kubwa ya watu na ni sehemu ya muqawama wa Lebanon katika kukabiliana na maghasibu wa Kizayuni; na inashiriki pia katika uga wa kisiasa wa nchi hiyo.

Salim Baddoura, balozi wa Lebanon UN

Viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kila mara wamekuwa wakitoa vitisho vya kuanzisha vita na mashambulio ya kijeshi dhidi ya Lebanon, na kutokana na vitisho hivyo, harakati ya Hizbullah, ambayo ni moja ya vikosi vya Lebanon na vya muqawama wa Kiislamu imekuwa ikijibu vitisho hivyo kwa kutangaza kuwa, endapo wazayuni watajaribu kurudia hatua kama waliyochukua katika vita vya siku 33, hatima mbaya sana itawafika wazayuni hao maghasibu.../