Wanamuqawama watungua 'drone' ya kijasusi ya Israel huko Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68028-wanamuqawama_watungua_'drone'_ya_kijasusi_ya_israel_huko_gaza
Wanamuqawama wa Palestina wamefanikiwa kutungua ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni wa Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 18, 2021 05:10 UTC
  • Wanamuqawama watungua 'drone' ya kijasusi ya Israel huko Gaza

Wanamuqawama wa Palestina wamefanikiwa kutungua ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni wa Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Duru za habari kutoka Palestina zinaarifu kuwa, drone hiyo ya kijasusi ya utawala haramu wa Israel ilitunguliwa usiku wa kuamkia leo na vikosi vya harakati za muqawama huko kaskazini mwa Gaza.

Wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina wamesema wametungua ndege hiyo isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni kwa kufanya ujasusi katika anga ya Ukanda wa Gaza.

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, ndege zisizo na rubani, ndege za kijeshi, helikopta na mizinga ya utawala wa Kizayuni imekuwa ikitumika kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza unaoshambulia na Wazayuni kila uchao

Tangu mwezi Disemba 2017 hadi hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya mashambulio ya mara kwa mara ya kikatili dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza.

Hadi hivi sasa maelfu ya Wapalestina wameshauawa shahidi na kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya kidhalimu ya utawala pandikizi wa Israel.