Jeshi la Israel lamuua shahidi kijana wa Kipalestina kwa kumpiga risasi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74150-jeshi_la_israel_lamuua_shahidi_kijana_wa_kipalestina_kwa_kumpiga_risasi
Askari wa utawala haramu wa Israel wamemuua shahidi kijana wa Palestina kwa kumpiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 31, 2021 22:53 UTC
  • Jeshi la Israel lamuua shahidi kijana wa Kipalestina kwa kumpiga risasi

Askari wa utawala haramu wa Israel wamemuua shahidi kijana wa Palestina kwa kumpiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Shirika rasmi la habari la Palestina WAFA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wanajeshi wa Israel walimpiga risasi barobaro huyo wa Kipalestina kwa jina la Raed Yousef Jadallah katika kijiji cha Beit Ur al-Tahta, magharibi mwa mji wa Ramallah.

Mashuhuda wanasema, baada ya kummiminia risasi kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 39, askari wa Israel walimuacha akavuja damu hadi akakata roho.

Wizara ya Afya ya Palestina imethibitisha kutoa mauaji hayo alfajiri ya leo Jumatano na kueleza kuwa, ni ya tatu ndani ya wiki moja huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Askari wa Israel wakimkandamiza kijana wa Kipalestina mjini Quds

Jumamosi iliyopita, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 12 wa Kipalestina aliyefahamika kama Omar Hasan Abu an-Neel aliaga dunia kutokana na majeraha ya risasi za Wazayuni, katika mji wa Malka, mashariki mwa jiji la Gaza.

Haya yanajiri wiki mbili baada ya wanajeshi hao makatili wa utawala haramu wa Israel kuwaua shahidi vijana wanne Wapalestina kwa kuwapiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.