Opereseheni ya kukomboa mji wa Falluja inaendelea nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7999-opereseheni_ya_kukomboa_mji_wa_falluja_inaendelea_nchini_iraq
Jeshi na vikosi vya wananchi vya Iraq wanaendelea na operesheni yao ya kuukomboa mji wa Falujja kutoka mikononi mwa genge la kigaidi la Daesh tangu siku sita zilizopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2016 23:21 UTC
  • Opereseheni ya kukomboa mji wa Falluja inaendelea nchini Iraq

Jeshi na vikosi vya wananchi vya Iraq wanaendelea na operesheni yao ya kuukomboa mji wa Falujja kutoka mikononi mwa genge la kigaidi la Daesh tangu siku sita zilizopita.

Katika operesheni ya jana Jumamosi, jeshi na vikosi vingine vya Iraq vilifanikiwa kuangamiza magaidi 110 wa Daesh na kujeruhi wengine wengi kaskazini mwa mji wa Falluja ambao ni ngome muhimu ya Daesh katika mkoa wa al Anbar wa magharibi mwa Iraq. Komandi ya opereseheni hiyo ya mjini Baghdad imetangaza pia kuwa, familia 507 zenye watu wapatao elfu mbili na 30 wameondolewa mjini humo kupitia njia zilizoandaliwa na jeshi la Iraq. Aidha askari wengine elfu tano wapya wametumwa huko Fallujja kushiriki kwenye operesheni hiyo muhimu. Operesheni ya kuukomboa mji wa Falluja ilianza siku ya Jumatatu kwa amri ya Haidar al Abadi, Waziri Mkuu wa Iraq. Operesheni za kuukomboa mji huo ambao hivi sasa umezingirwa kila upande na vikosi vya serikali na vya wananchi wa Iraq, zimeshapelekea kukombolewa zaidi ya maeneo 19 kutoka mikononi mwa Daesh na kuangamiza idadi kubwa ya magaidi. Meja Jenerali Shaker Joudeh, mkuu wa polisi ya fiderali ya Iraq amesema kuwa, jeshi la polisi la nchi hiyo limefanikiwa kuondoa raia 760 kutoka Falluja tangu operesheni hiyo ianze siku ya Jumatatu.