Al Nujaba: Harakati za Uturuki nchini Iraq ni tishio
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81120-al_nujaba_harakati_za_uturuki_nchini_iraq_ni_tishio
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchini Iraq ya al Nujaba amesema kuwa harakati za Uturuki huko Iraq ni tishio; na kwamba iwapo nchi hiyo haitaacha chokochoko zake hizo basi Wairaki wataingia katika hali ya kijeshi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 07, 2022 12:10 UTC
  • Al Nujaba: Harakati za Uturuki nchini Iraq ni tishio

Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchini Iraq ya al Nujaba amesema kuwa harakati za Uturuki huko Iraq ni tishio; na kwamba iwapo nchi hiyo haitaacha chokochoko zake hizo basi Wairaki wataingia katika hali ya kijeshi.

Uturuki katika miaka ya karibuni imeishambulia Iraq mara kadhaa kwa kisingizio cha kuwaangamiza wapiganaji wa chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi wa Uturuki cha PKK. Uvamizi huo umekabiliwa na radiamali kali ya serikali ya Iraq na ya nchi nyingine mbalimbali duniani. 

Wapiganaji wa PKK 

Ofisi ya Habari ya Harakati ya al Nujaba imeripoti kuwa, msemaji wa harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu ya Iraq Nasr al Shammary amekosoa vikali uvamizi na vitisho vya jeshi la Uturuki na kutahadharisha kuwa hatua ya jeshi vamizi la Uturuki ya kujenga kambi za kijeshi huko Iraq inawachochea Wairaqi kuchukua hatua. 

Kuhusu masuala ya ndani ya Iraq, Al Shammary amesema: Inapasa kutilia maanani kwamba mwanajeshi yoyoye nchini Iraq anaruhusiwa kutumia silaha yake kulinda itikadi yake, matukufu na usalama wa taifa.   

Al Shammary ameiusia serikali ya Iraq ijiepushe na kuegemea upande wowote katika mizozo ya kimataifa na badala yake idhamini maslahi ya taifa kwa kushirikiana na nchi zenye nia ya kushirikiana.