Jihadul Islami: Operesheni dhidi ya Israel ni jibu kwa jinai zake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82008-jihadul_islami_operesheni_dhidi_ya_israel_ni_jibu_kwa_jinai_zake
Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema operesheni za hivi karibuni za wanamuqawama wa Kipalestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ni jibu kwa jinai za utawala huo pandikizi na hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na Tel Aviv.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 31, 2022 22:59 UTC
  • Jihadul Islami: Operesheni dhidi ya Israel ni jibu kwa jinai zake

Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema operesheni za hivi karibuni za wanamuqawama wa Kipalestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ni jibu kwa jinai za utawala huo pandikizi na hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na Tel Aviv.

Katika mahojiano na shirika la habari la Iran Press, Khalid al-Batsh, kiongozi wa ngazi ya juu wa Jihadul Islami amesema operesheni ya mwanamapambano wa Palestina huko Bnei Brak, mashariki mwa Tel Aviv siku chache zilizopita inaonesha wazi kuwa Wapalestina hawajasalimu amri mbele ya mashinikizo, na wanaendelea na njia ya muqawama.

Amesisitiza kuwa, madhali utawala haramu wa Israel unaendelea kuua viongozi wa Kipalestina, unapaswa kufahamu kuwa hakuna shaka kuwa hauwezi kuepuka visasi vya wanamuqawama.

Jumanne iliyopita eneo hilo la "Bnei Brak" lilishuhudia operesheni ya kijasirii iliyofanywa na mwanamapambano wa Palestina, Zia Hamarsheh, ambaye aliuawa shahidi. Wazayuni 5 waliangamizwa na wengine 6 walijeruhiwa katika operesheni hiyo. 

Siku ya Ardhi ya Palestina huadhimishwa Machi 30 kila mwaka

Kabla ya hapo, askari wawili wa jeshi la utawala haramu wa Israel waliangamizwa, huku wengine 12 wakijeruhiwa katika operesheni nyingine katika mji wa Al-Khadira, kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kuhusu Siku ya Ardhi ya Palestina ambayo iliadhimishwa juzi Machi 30, kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema: Wapalestina wamejitolea kupigania haki zao ndani ya ardhi yao, na jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za kuuondolea mzingiro Ukanda wa Gaza, sanjari na kutetea haki za Wapalestina.