Israel inawapelekea 'futari' wapiganaji wa Daesh huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i8908-israel_inawapelekea_'futari'_wapiganaji_wa_daesh_huko_syria
Imerifiwa kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unawapelekea misaada ya chakula wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika maeneo ambayo yako chini ya udhibiti wao nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2016 09:52 UTC
  • Israel inawapelekea 'futari' wapiganaji wa Daesh huko Syria

Imerifiwa kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unawapelekea misaada ya chakula wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika maeneo ambayo yako chini ya udhibiti wao nchini Syria.

Jafar Miya, mwanaharakati katika eneo la Quneitra kusini mwa Syria ameliambia shirika la habari la Tasnim kuwa, magaidi wa Daesh wamekuwa wakipokea shehena za chakula kutokana utawala haramu wa Israel. Amesema baadhi ya vyakula hivyo vimepakiwa kwenye mifuko yenye nembo za makampuni ya utawala huo ghasibu.

Duru za habari zimearifu kuwa, mbali na kupokea misaada ya chakula, wapiganaji wa Daesh wamekuwa wakitibiwa katika hospitali za Israel. Nyaraka kutoka hospitali za Israel zimefichua kuwa, jeshi la utawala huo wa Kizayuni limekuwa likigharamia malipo ya kutibiwa wanachama wa Daesh. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, aghalabu ya magaidi wa Daesh wanapopata majeraha huwa wanatibiwa katika hospitali ya Galil, iliyoko katika mji wa pwani wa Nahariya, kaskazini mwa ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Serikali ya Damascus imekuwa ikisisitiza kuwa, kushamiri na kuenea makundi ya kitakfiri na kigaidi kumevuruga amani ya eneo la Mashariki ya Kati na kudhamini usalama wa utawala wa Kizayuni. Jeshi la Syria limenasa idadi kubwa ya silaha zilizoundwa na utawala haramu wa Israel toka mikinoni mwa matakfiri wa Daesh tangu walipoanzisha harakati zao za kigaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu Machi mwaka 2011.