Raia 30 wauawa katika hujuma ya Daesh nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i8932-raia_30_wauawa_katika_hujuma_ya_daesh_nchini_iraq
Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa wimbi la hujuma za kitatili na za ulipizaji kisasi za Daesh (ISIS), wanachama wa kundi la hilo la kigaidi na kitakfiri wamewaua kwa kufyatulia risasi raia zaidi ya 30 magharibi mwa mji wa Fallujah, mkoa wa al-Anbar.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2016 02:36 UTC
  • Raia 30 wauawa katika hujuma ya Daesh nchini Iraq

Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa wimbi la hujuma za kitatili na za ulipizaji kisasi za Daesh (ISIS), wanachama wa kundi la hilo la kigaidi na kitakfiri wamewaua kwa kufyatulia risasi raia zaidi ya 30 magharibi mwa mji wa Fallujah, mkoa wa al-Anbar.

Kamandi ya Operesheni za Pamoja ya Iraq imesema kuwa, wanamgambo wa Daesh jana Ijumaa waliwaua kwa kuawamiminia risasi watu zaidi ya 30 wa makabila ya Albu Saleh na Albu Hatam, walipokuwa wakiukimbia mji wa Fallujah wakielekea mji wa al-Amiriyah, yapata kilomita 69 magharibi mwa mji mkuu Baghdad. Taarifa ya Kamandi ya Operesheni za Pamoja ya Iraq imesema kuwa, aghalabu ya waliouawa katika hujuma hiyo ya kikatili ni wanawake na watoto wadogo. Haya yanajiri siku mbili baada ya miripuko miwili ya kigaidi kuutikisa mji wa Baghdad na kusababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa wengine wengi. Mashambulio hayo ya ulipizaji kisasi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh yameshadidi kufuatia operesheni za jeshi la Iraq kwa kushirikiana na harakati za kujitolea za wananchi 'Hashdu ash-Shabi' kupata mafanikio makubwa katika operesheni za kuukomboa mji wa kistratijia wa Fallujah mkoani al-Anbar, magharibi mwa nchi hiyo.