Wazayuni wanaona bora Daesh kuliko Bashar al Assad
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9811-wazayuni_wanaona_bora_daesh_kuliko_bashar_al_assad
Shirika la ujasusi wa kijeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja uungaji mkono wake kwa genge la kitakfiri la Daesh na kutangaza kuwa, kundi hilo ni bora kwa utawala huo kulikoni serikali ya Rais Bashar al Assad huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2016 11:23 UTC
  • Wazayuni wanaona bora Daesh kuliko Bashar al Assad

Shirika la ujasusi wa kijeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja uungaji mkono wake kwa genge la kitakfiri la Daesh na kutangaza kuwa, kundi hilo ni bora kwa utawala huo kulikoni serikali ya Rais Bashar al Assad huko Syria.

Mtandao wa habari wa televisheni ya al Alam umemnukuu Meja Jenerali Herzl Halevy, mkuu wa shirika la ujasusi wa kijeshi la utawala wa Kizayuni akizungmzia kushinda vibaya hivi karibuni magaidi wa ISIS na kusisitiza kuwa, Israel haipendi kuona kundi la Daesh linashindwa, kwani kushindwa kundi hilo kutaiweka Israel katika wakati mgumu sana.

Herzl Halevy amesema wazi tena bila ya kificho kuwa, utawala wa Kizayuni unaona bora kundi la Daesh kuliko serikali ya Syria.

Kwa upande wake mtandao wa habari wa Russia Today umemnukuu Herzl Halevy akisema, Israel itatumia nguvu zake zote kuhakikisha kuwa kundi la Daesh halishindwi nguvu.

Kabla ya hapo viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwahi kutangaza kuwa, wanastahabu na wanaona bora kutekwa ardhi nzima ya Syria na kundi la Daesh na kuondolewa madarakani serikali ya Rais Bashar al Assad kutokana na kuwa serikali hiyo ni muitifaki wa Iran.