-
Afisa wa UN: Ni vigumu kupeleka misaada Gaza
Dec 25, 2024 00:05Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa imekuwa vigumu kufikisha hata msaada mdogo kwa raia wa Palestina huko Ukanda wa Gaza.
-
Oxfam: Katika muda wa miezi miwili na nusu malori 12 tu ya chakula na maji yamefika kaskazini ya Ghaza
Dec 24, 2024 08:56Shirika la misaada ya kibinadamu la Uingereza la Oxfam limetangaza kuwa, katika muda wa miezi miwili na nusu, ni malori 12 pekee yamesambaza chakula na maji katika eneo la kaskazini mwa Ghaza na kutahadharisha kuwa hali ya kibinadamu katika eneo hilo la Palestina ni mbaya sana.
-
Al-Qassam yawaangamiza askari watatu wa jeshi la Kizayuni kaskazini mwa Ghaza
Dec 24, 2024 08:20Wapiganaji wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wametangaza kuwa wametekeleza operesheni tata kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza na kufanikiwa kuwaangamiza wanajeshi kadhaa wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
HAMAS: Wapalestina wapambane kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Palestina
Dec 24, 2024 08:19Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa wito wa kufanyika "hamasa kubwa ya umma" kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
-
UN yaonya kuhusu hatari ya kuenea mapigano kaskazini mashariki mwa Syria
Dec 24, 2024 03:20Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria ameonya kuhusu kuenea migogoro na mapigano, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo baada ya kupinduliwa serikali ya Rais Bashar al Assad.
-
Utawala wa Kizayuni wakiri kuwa ndio uliomuua kigaidi Ismail Haniyeh
Dec 24, 2024 03:17Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni kwa mara ya kwanza amekiri kwamba israel ndiyo iliyomuua kigaidi Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS, Ismail Haniyeh mjini Tehran.
-
Hamas yalaani vikali kushambuliwa hospitali Gaza; yasema Israel inafanya maangamizi ya kizazi
Dec 23, 2024 23:05Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza na kusema kuwa, huo ni "uhalifu usio na mfano dhidi ya binadamu."
-
UNICEF: Watoto 14500 wameuawa shahidi hadi sasa katika Ukanda wa Gaza
Dec 23, 2024 10:47Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuuawa shahidi watoto 14,500 wa Kipalestina huko Gaza.
-
Wananchi wa Uturuki waandamana kulaani jinai za Israel Gaza
Dec 23, 2024 10:33Maelfu ya wananchi wa Uturuki wameandamana katika mji muhimu wa nchi hiyo Istanbul na kutangazza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza.
-
Wazayuni wayafanya maisha kuwa magumu huko Jabalia, Ukanda wa Gaza
Dec 23, 2024 10:31Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameifanya hali ya mambo na maisha kuwa ngumu katika eneo la Jabalia kwa lengo la kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Kipalestina wa mji huo.