-
Yemen yawaasa Waislamu wasusie bidhaa za Israel, Marekani
Mar 11, 2024 07:54Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ametoa mwito kwa mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kususia bidhaa zinazozalishwa na Israel na Marekani, akisisitiza kuwa hatua hiyo itakuwa ni zawadi ndogo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanaoendelea kuuawa kikatili na utawala wa Kizayuni.
-
Syria: Kuunga mkono jinai za Netanyahu kumefichua dhati ya Wamagharibi
Mar 11, 2024 07:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amezikosoa vikali nchi za Magharibi kwa kuendelea kuunga mkono jinai za kivita zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, uungaji mkono huo umefichua dhati halisi ya Wamagharibi.
-
Muigizaji wa kimataifa Khaled Abdullah: Ramadhani itukumbushe njaa ya watu wa Gaza
Mar 11, 2024 04:39Muigizaji wa Uingereza mwenye asili ya Misri, Khaled Abdullah, ametuma ujumbe wa kuwaunga mkono watu wa Palestina kupitia akaunti yake kwenye jukwaa la "X", akisema mwanzo wa mwezi wa Ramadhani ni fursa ya kukumbuka mateso ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kuwaokoa kutokana na njaa.
-
Hamas: Hakuna makubaliano kabla ya kusitisha kikamilifu uvamizi wa Israel, kuondoka Gaza
Mar 11, 2024 04:39Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema hakutakuwa na makubaliano yoyote na utawala wa katili wa Israel kabla ya kusimamisha kikamilifu hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuyaondoa majeshi yake katika eneo hilo.
-
Wapalestina waanza mfungo wa Ramadhani katika hali ya vita
Mar 11, 2024 00:51Wapalestina wameanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani katika hali ya huzuni na hatua zilizoimarishwa za usalama na polisi ya utawala haramu wa Israel. Hii ni katika hali ambayo, mazungumzo ya kupatikana muafaka wa kusitishwa mapigano yamekwama.
-
Waliouawa shahidi Gaza wakaribia 32,000; Israel yaendeleza mashambulizi ya kinyama
Mar 11, 2024 00:50Duru za afya katika Ukanda wa Gaza huko Palestina zimetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kufuatia mashambulio ya kinyama ya Israel imekaribia 32,000.
-
Mfungwa wa zamani: Jela za Israel 'ni za kikatili zaidi' kuliko jela za Marekani za Guantanamo, Abu Ghraib
Mar 11, 2024 04:40Mfungwa wa zamani wa Kipalestina amesema kinachoendelea kwa Wapalestina katika jela za Israel ni "ukatili mkubwa" zaidi kuliko jinsi wafungwa walivyotendewa katika jela za Marekani za Guantanamo Bay kusini mashariki mwa Cuba na Abu Ghraib nchini Iraq.
-
Wafanyakazi wa UNRWA waliteswa ili wakiri uwongo dhidi ya Hamas
Mar 10, 2024 08:30Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina (UNRWA) limekusanya ripoti kuhusu jinai za Tel Aviv dhidi ya haki za binadamu katika vita dhidi ya Ukanda wa Gaza, na kufichua "mateso na dhuluma" walizofanyiwa wafanyakazi wa shirika hilo katika jela za utawala ghasibu wa Israel ili wakiri tuhuma bandia dhidi ya Hamas.
-
Kukosolewa propaganda za Marekani kuhusiana na misaada ya kibinadamu
Mar 10, 2024 07:50Akihutubia bunge la Marekani siku ya Alkhamisi, Rais Joe Biden alisema ameliamuru jeshi la nchi hiyo kuweka bandari kwenye pwani ya Gaza katika Bahari ya Mediterania.
-
Kiongozi wa Hamas ahimiza hatua za haraka zichukuliwe kumaliza vita vya Gaza kabla ya Ramadhani
Mar 10, 2024 03:14Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ametoa wito wa kufanyika juhudi za haraka katika ulimwengu wa Kiislamu ili kulazimisha kusitishwa vita huko Gaza katika siku zilizosalia kabla ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.