Mar 29, 2024 11:58 UTC
  • CDC: Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yameongezeka sana Marekani

Mambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) yanaonekana kuongezeka kwa kiwango cha kuogofya miongoni mwa watu wazima nchini Marekani.

Takwimu mpya za Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini humo (CDC) zinaonyesha kuwa, maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na klamidia (chlamydia) yameongezeka maradufu miongoni mwa watu wenye umrii wa miaka 55 na zaidi katika kipindi cha miaka 10 baina ya 2012 na 2022.

Justyna Kowalska, mwandishi wa makala kuhusu utafti huo, ambaye pia ni profesa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Warsaw ameonya kuwa, madaktari na watu wazima nchini Marekani wanapuuza maambukizi miongoni mwa watu wenye miaka zaidi ya 55.

Prof Kowaska ameeleza kuwa: Tunazungumza kuhusu uvutaji wa sigara, lishe, mazoezi, na mambo mengine mengi, lakini hatuzungumzii kabisa juu ya ngono (zembe).

Ukimwi ungali mgogoro mkubw wa kiafya nchini Marekani

Madaktari nchini Marekani wameonya kuwa, ueneaji wa kasi wa magonjwa ya zinaa miongoni mwa watu wazima umechangiwa pakubwa na kudhoofika mfumo wa kinga ya mwili wa watu wa tabaka hilo.

Si vibaya kuashiria hapa kuwa, maambukizi ya maradhi ya zinaa hususan chlamydia miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 45 na zaidi yaliongezeka kwa asilimia 22 nchini Uingereza mwaka 2022.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa, kampeni kubwa ya kushajiisha ndoa na mahusiano ya kishoga ya watu wenye jinsia moja imechangia pakubwa ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya zinaa katika nchi za Magharibi.

Tags