Ubelgiji yalaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115528-ubelgiji_yalaani_jinai_za_utawala_haramu_wa_israel_dhidi_ya_gaza
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ubelgiji imelaani shambulizi la Israel dhidi ya makazi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Aug 22, 2024 23:25 UTC
  • Ubelgiji yalaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ubelgiji imelaani shambulizi la Israel dhidi ya makazi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Utawala ghasibu wa Kizayuni juzi Jumatano uliishambulia shule ya Salahuddin yenye mfungamano na shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA huko magharibi mwa Gaza.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ubelgiji sambamba na kutoa taarifa ya kulaani jinai hiyo imesisitizia haja ya kusitishwa kwa mashambulizi dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza.

Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Ubelgiji imetangaza kuwa sheria za kimataifa za kibinadamu zinapaswa kuheshimiwa katika Ukanda wa Gaza na usitishaji vita unapaswa kuanzishwa haraka iwezekanavyo.

 

Louise Waterridge, Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina (UNRWA), ametahadharisha kuhusu kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusema: Vifo ni hatima pekee inayowakabili watu wa Gaza na kuwa hakuna njia nyingine ya kuepuka jinai zisizo na kikomo za utawala huo.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika shule ya Salahuddin magharibi mwa mji wa Gaza ni muendelezo wa oparesheni za mauaji ya kimbari zinazotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.