Mwendesha Mashtaka wa ICC asisitiza Netanyahu na Gallant wakamatwe haraka iwezekanavyo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115588-mwendesha_mashtaka_wa_icc_asisitiza_netanyahu_na_gallant_wakamatwe_haraka_iwezekanavyo
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amewataka majaji wa mahakama hiyo watoe haraka waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa vita wa utawala huo Yoav Gallant.
(last modified 2026-04-23T06:05:17+00:00 )
Aug 24, 2024 06:33 UTC
  • Mwendesha Mashtaka wa ICC asisitiza Netanyahu na Gallant wakamatwe haraka iwezekanavyo

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amewataka majaji wa mahakama hiyo watoe haraka waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa vita wa utawala huo Yoav Gallant.

Kwa mujibu wa IRNA, Karim Khan amesema ICC inayo mamlaka kisheria ya kushughulikia uhalifu wa kivita wa Waisrael na akawataka majaji wa mahakama hiyo wachukue uamuzi haraka iwezekanavyo kuhusiana na kutiwa nguvuni Netanyahu na Gallant.
 
Khan amesisitiza kuwa: ucheleweshaji wowote usio na msingi wa kushughulikia uhalifu huo wa kivita unakandamiza haki za wahanga na waathirika wa jinai hizo.
 
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC amesema, kuna sababu za kimantiki zinazothibitisha kuwa Netanyahu anahusika na jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na akakumbusha kwamba, hakuna mpaka wa muhula uliowekwa kwa majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai wa kuamua kuhusu utoaji waranti wa kukamatwa viongozi hao wa utawala wa Kizayuni.
Image Caption

Karim Khan anataka viongozi wakuu wa utawala wa Kizayuni watiwe nguvuni kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kuwalenga na kuwashambulia makusudi raia wa Palestina.

 
Mwezi uliopita, Netanyahu alitoa mjibizo kuhusiana na kuchunguzwa jinai za Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na kudai kwamba hatua hiyo ni sawa na kuitusi historia. 
 
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na nchi za Magharibi, utawala ghasibu wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.
 
Takwimu za karibuni za Wizara ya Afya ya Palestina zinaonyesha kuwa zaidi ya Wapalestina 40,265 wameuawa shahidi katika Ukanda wa Ghaza na wengine zaidi ya 93,000 wamejeruhiwa.../