Daily Mail: Trump amekwama kwenye kinamasi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137408-daily_mail_trump_amekwama_kwenye_kinamasi
Gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa Iran imethibitisha kuwa ina nguvu na imejiandaa vizuri sana kuliko vile ilivyokuwa ikidhaniwa na Marekani.
(last modified 2026-03-16T10:32:54+00:00 )
Mar 16, 2026 10:32 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa Iran imethibitisha kuwa ina nguvu na imejiandaa vizuri sana kuliko vile ilivyokuwa ikidhaniwa na Marekani.

Weledi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa hatua ya Tehran ya kufunga Lango Bahari la Hormuz ili kujibu uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ilikuwa sahihi kikamilifu na imezima njama za Tel Aviv na Washington za kutaka kuukalia kwa mabavu Mlango Bahari huo. 

Gazeti la Daily Mail limeakiri kuwa, wiki mbili baada ya kushambuliwa Iran, Rais Donald Trump wa Marekani alisema kuwa Washington tayari imeshinda huku ukweli wa mambo ukiwa mchungu sana kwa nchi yake. Daily Mail limeandika: Maafa ya vita yamewaathiri wakulima wa Marekani ambao wanategemea kuuza mazao yao katika Ghuba ya Uajemi. Limeendelea kuandika: Iran imethibitisha kuwa ni imara sana na imejiandaa vizuri kuliko Marekani ilivyokuwa ikifikiria na kwamba matarajio ya Trump ya kupata ushindi haraka na mkubwa baada ya kuuliwa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu yameyoyoma. 

Wakati huo huo, Robert Peep mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Chicago amekiri kuwa hali ya kijiografia ya Asia Maghaibi ni kwa maslahi ya Iran. Amesema njia ya kupita meli katika Lango Bahari la Hormuz ni nyembamba sasa jambo linalopelekea usindikizaji meli baharini kuwa shabaha rahisi kwa droni na mabomu ya Iran.

Ameongeza kuwa: Trump amenaswa katika mivutano mikubwa na kwamba kung'ang'ania kwake kuendelea na vita hivi kunatatiza zaidi hali ya mambo.