Dec 31, 2016 14:59 UTC
  • Daktari aliyenajisi makumi ya wagonjwa afikishwa mahakamani Ufaransa

Daktari wa Ufaransa aliyewabaka waonjwa 37 katika mji wa Cher amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Daktari huyo mwenye umri wa miaka 67 mbali na kubaka wanawake wagonjwa vilevile alikuwa akipiga picha baadhi ya uhalifu wake.  

Ripoti zinasema umri wa baadhi ya wahanga wa daktari huyo ulikuwa chini ya umri  wa kisheria wakati alipowabaka na kuwajanisi.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa mwaka 2014 baada ya wagonjwa wawili kuwasilisha mashtaka na mmoja wao wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18.

Kesi za ubakaji zimekithiri sana barani Ulaya

Ripoti za ubakaji barani Ulaya zimekuwa habari motomoto katika vyombo vya habari. Pamoja na hayo kashfa za makocha na walimu wa mpira wa miguu kuwabaka vijana na mabarobaro katika vilabu vya mpira wa soka nchini Uingereza ndizo zilitikisa zaidi vyombo vya habari na kuzua mshtuko mkubwa. 

Tags