Iran: Mataifa yote yanapaswa kuzuia kutokea maafa ya kibinadamu Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34015-iran_mataifa_yote_yanapaswa_kuzuia_kutokea_maafa_ya_kibinadamu_myanmar
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi mkubwa alionao kutokana na hali mbaya na ya kusikitisha wanayokabiliwa nayo Waislamu wa Myanmar na kuelezea juu ya kuundwa kundi ma mawasiliano la nchi za Kiislamu katika siku za usoni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 07, 2017 00:08 UTC
  • Iran: Mataifa yote yanapaswa kuzuia kutokea maafa ya kibinadamu Myanmar

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi mkubwa alionao kutokana na hali mbaya na ya kusikitisha wanayokabiliwa nayo Waislamu wa Myanmar na kuelezea juu ya kuundwa kundi ma mawasiliano la nchi za Kiislamu katika siku za usoni.

Gholamali Khoshroo, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali duru mpya ya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wa Myanmar na kusema kuwa,mataifa yote yanapaswa kufanya juhudi za kuzuia kutokea maafa ya kibinadamu nchini Myanmar ambapo Waislamu wa jamii ya Rohingya wamekuwa wakihujumiwa na kuuawa.

Gholamali Khoshroo, amesema kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya kwa karne nyingi wamekuwa wakiishi nchini Myanmar lakini sasa wananyimwa haki ya kimsingi kabisa nayo ni haki ya uraia. 

Gholamali Khoshroo, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, jeshi la Myanmar na waungaji mkono wake wamechoma moto maelfu ya nyumba za Waislamu katika jimbo loa Rakhine na kuwafanya mamia ya maelfu ya Waislamu hao kuwa wakimbizi.

Zaidi ya Waislamu 400 Warohingya wa jimbo la Rakhine lililoko magharibi mwa Myanmar wameuawa katika mashambulio ya jeshi la nchi hiyo yaliyoanza tarehe 25 ya mwezi uliopita wa Agosti. Serikali ya Myanmar inawahesabu Waislamu wapatao milioni moja Warohingya kuwa ni wahajiri haramu na wala haiwapi haki zozote za kiraia.

Umoja wa Mataifa umeendelea kukosolewa kutokana na kutochukua hatua za maana za kuhitimisha mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu hao wasio na hatia.