Macron aitaka Saudia iache kuyafadhili kifedha makundi ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37003-macron_aitaka_saudia_iache_kuyafadhili_kifedha_makundi_ya_kigaidi
Rais wa Ufaransa amesema kuwa Saudi Arabia inapasa kuacha kuyafadhili kifedha makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 30, 2017 12:49 UTC
  • Macron aitaka Saudia iache kuyafadhili kifedha makundi ya kigaidi

Rais wa Ufaransa amesema kuwa Saudi Arabia inapasa kuacha kuyafadhili kifedha makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Emmauel Macron amesema kuwa Paris itawakabidhi viongozi wa Saudia orodha ya majina ya makundi ya kigaidi ili Riyadh iache kuyafadhili kifedha makundi hayo. 

Katika mahojiano yake na televisheni ya France 24, Rais wa Ufaransa alizungumzia pia Iran na kusema kuwa, Paris iko katika fremu ya mapatano na Iran na kwamba Ufaransa itaendelea kuheshimu majukumu yake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. 

Rais Macron wa Ufaransa pia amelaani biashara ya utumwa huko Libya na kueleza kuwa kuna udharura wa kutumia nguvu za kijeshi kwa ajili ya kupambana na wafanya magendo ya binadamu huko Libya. 

Wahajiri wa Kiafrika katika harakati za kuelekea Ulaya 

Ameongeza kuwa, kunapaswa kuandaliwa uwanja wa kuwarejesha makwao raia wa Kiafrika waliopo makambini huko Libya kwa mashirikiano na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji.