Russia yaionya Marekani kuhusu kuchochea mgogoro wa Korea
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37485-russia_yaionya_marekani_kuhusu_kuchochea_mgogoro_wa_korea
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameionya Marekani kwa siasa zake za kuchochea na kushadidisha mgogoro wa Rasi ya Korea.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 12, 2017 02:36 UTC
  • Russia yaionya Marekani kuhusu kuchochea mgogoro wa Korea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameionya Marekani kwa siasa zake za kuchochea na kushadidisha mgogoro wa Rasi ya Korea.

Sergey Lavrov amesema katika kikao cha pande tatu cha mawaziri wa mambo ya nje wa India, China na Russia kilichofanyika Jumatatu mjini New Delhi India, kwamba, Moscow ina wasiwasi na siasa za Marekani za kushadidisha mgogoro wa Peninsula ya Korea na kuufikisha katika kiwango cha hatari.

Amesema, hakuna nchi yoyote kati ya nchi tatu za India, China na Russia inayofurahishwa na kuendelea mgogoro wa Korea Kaskazini.

Kwa upande wake, mwanasheria mmmoja wa Russia amesema, hivi sasa Korea Kaskazini inajiandaa kufanyia majaribio kombora lake jingine la masafa marefu ambalo linaweza kuipiga Marekani.

Ni hivi majuzi tu ambapo kundi moja la wabunge wa Russia lilielekea Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini katika juhudi za kutatua mgogoro wa nchi hiyo.

Makombora ya Korea Kaskazini

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia amesema, nchi yake pamoja na China na India ziko tayari kutoa utaalamu wao kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ugaidi na kupambana na vyanzo vya kifedha vinavyotumiwa na magaidi katika nchi mbalimbali duniani.

Amesema, Russia imeandaa orodha maalumu ya kushirikiana na China na India katika uwanja huo.