Umoja wa Mataifa: Tunapinga Marekani kuhamishia ubalozi wake Beitul-Muqadas
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwa mara nyingine tena upinzani wa taasisi hiyo kwa uamuzi wa Marekani wa kutaka kuhamishia ubalozi wake katika mji wa Beitul-Muqaddas huko Palestina inayokkaliwa kwa mabavu.
Stéphane Dujarric, msemaji wa Antoni Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo sambamba na kuashiria uungaji mkono wake kwa haki ya kujitawala ya nchi wanachama wa umoja huo amesisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa unapinga uamuzi wa upande mmopja wa Marekani wa kutakka kuhamishia ubalozi wake katika mji wa Beitul-Muqaddas.
Msemaji huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba, taasisi hiyo haikubaliani na uamuzi huo wa Rais Donald Trump wa Marekani.
Wakati huo huo, balozi wa Palestina katika Umoja wa Ulaya amesisitiza juu ya udharura wa nchi za umoja huo kuitambua rasmi Palestina na hiyo kuwa kama hatua ya kwanza ya kupinga maamuzi ya Washington dhidi ya Quds Tukufu.
Itakumbukwa kuwa, tarehe 6 Disemba mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani alichukua hatua ya kuitangaza Quds Tukufu kuwa eti mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
Aidha rais huyo wa Marekani alitangaza kuwa serikali ya Washington imeanzisha mchakato wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji huo kutoka Tel Aviv. Kuitambua rasmi Quds inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel kuwa mji mkuu wa utawala huo ni kinyume kabisa na maazimio ya kimataifa.