Jul 13, 2018 04:12 UTC
  • Trump akaribishwa London kwa wimbi kubwa la maandamano

Rais Donald Trump wa Marekani aliwasili London, mji mkuu wa Uingereza na kukaribishwa kwa wimbi kubwa la maandamano ya wananchi waliokuwa na hasira ambao wanapinga safari yake.

Taarifa zinasema baada ya Trump kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Stansted mjini London kwa ziara ya siku nne nchini Uingereza , maelfu ya watu waliandamana huku wakitoa nara dhidi ya mtawala huyo wa Marekani na sera zake.

Aidha pamoja na kuwepo ulinzi mkali, baadhi ya waandamanaji walifanikiwa kufika karibu na ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza kubainisha upinzani wao kwa safari hiyo.

Waandamanaji wengine pia walifika mbele ya nyumba ya balozi wa Marekani katikati mwa London na kushiriki katika maandamano dhidi ya Trump.

Maandamano wakati helikopta iliyombeba Trump ikipita sehemu moja ya London, 12.07.2018

Waandaamanaji walikuwa wamebebea mabango yenye maandishi kama vile , 'La Kwa Trump, La Kwa Ubaguzi' na 'Trump Hakaribishwi Hapa."

Trump anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May leo Ijumaaa na pia atakutana na Malikia Eliabeth wa nchi hiyo. Kutokana na hofu ya maandamano makubwa zaidi ya wananchi wenye hasira, mikutano hiyo imepangwa kufanyika nje ya London.

Tags