Waziri wa Sheria Marekani aamuru kutimuliwa haraka wahajiri
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47515-waziri_wa_sheria_marekani_aamuru_kutimuliwa_haraka_wahajiri
Waziri wa Sheria wa Marekani ameendeleza siasa za serikali ya nchi hiyo ya kupiga vita wahajiri kwa kutoa amri ya kufukuzwa haraka wahajiri haramu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 17, 2018 23:45 UTC
  • Waziri wa Sheria Marekani aamuru kutimuliwa haraka wahajiri

Waziri wa Sheria wa Marekani ameendeleza siasa za serikali ya nchi hiyo ya kupiga vita wahajiri kwa kutoa amri ya kufukuzwa haraka wahajiri haramu nchini humo.

Jeff Sessions ametoa amri hiyo akizihutubu mahakama za Marekani, ambapo hata hivyo amekabiliwa na ukosoaji mkali. Kwa mujibu wa amri hiyo, vituo vyote vilivyo chini ya vyombo vya mahakama vinavyohusika na masuala ya wahamiaji, vimetakiwa kuacha kuchelewesha mwenendo wa uchunguzi wa kesi za wahajiri. Kwa upande wake Stephen Canc, mmoja wa mawakili wa wahajiri ameitaja amri mpya ya Waziri wa Sheria wa Marekani kuwa ni tatizo kubwa.

Rais Donald Trump wa Marekani

Mahakama zinazohusika na masuala ya wahajiri ziko chini ya usimamizi wa Wizara ya Sheria ya Marekani ambapo hata mwendesha mashtaka mkuu anaweza kuingilia mambo yake. Hii sio mara ya kwanza kwa Jeff Sessions kuingilia mambo ya ndani ya mahakama hizo, suala ambalo halikuwahi kushuhudiwa kwa mawaziri wengine wa Sheria wa serikali zilizopita nchini Marekani. Serikali ya Rais Donald Trump imekuwa ikitekeleza sera za kibaguzi za kuwaondoa wahajiri au kuwazuia kuingia nchi hiyo. Kwa mujibu wa sera hizo, zaidi ya watoto 1,300 wa wahajiri walitenganishwa na wazazi wao, na kungali kuna zaidi ya 500 ambao bado hawajarejeshwa kwa wazazi wao.