Ufaransa yafanya njama za kujipenyeza zaidi bara la Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48932-ufaransa_yafanya_njama_za_kujipenyeza_zaidi_bara_la_afrika
Ufaransa na katika fremu ya kupenyeza zaidi ndani ya bara la Afrika imetangaza utayarifu wake kwa ajili ya kupambana na kile kilichosemwa kuwa ni ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 20, 2018 23:05 UTC
  • Ufaransa yafanya njama za kujipenyeza zaidi bara la Afrika

Ufaransa na katika fremu ya kupenyeza zaidi ndani ya bara la Afrika imetangaza utayarifu wake kwa ajili ya kupambana na kile kilichosemwa kuwa ni ugaidi.

Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa aliyasema hayo alipokutana na Roch Marc Christian Kaboré, Rais wa Burkina Faso na kuongeza kuwa, serikali ya Paris imejiandaa kuisaidia nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika kuidhaminia usalama na kupambana na ugaidi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa kikosi cha kundi la nchi tano za sahel mwa Afrika kinachozijumuisha nchi za Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad.

Kikosi cha kundi la nchi tano za sahel mwa Afrika kiliundwa mwaka 2014 na tarehe sita mwaka jana sambamba na kupitishwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, iliamuliwa kuundwa kikosi cha pamoja kwa ajili ya kukabiliana na machafuko, makundi yenye misimamo mikali na ugaidi.

Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Ulinzi wa Mambo ya Nje wa Ufaransa na Roch Marc Christian Kaboré, Rais wa Burkina Faso

Tangu katikati ya mwaka 2013 askari wa Ufaransa na kupitia kile kilichosemwa kuwa eti ni kupambana na ugaidi kilitia nanga katika baadhi ya nchi za Afrika, hata hivyo licha ya kutokuwa na mafanikio yoyote katika kuimarisha usalama na kuondoa tishio la ugaidi, hawakuondoka katika bara hilo. Burkina Faso imekuwa ikishuhudia machafuko na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2015 na kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa nchi hiyo, hadi sasa zaidi ya watu 230 wamepoteza maisha. Madola ya Magharibi yamekuwa yakitumia suala la kupambana na ugaidi kwa ajili ya kupenyeza ndani ya nchi mbalimbali za dunia kwa lengo la kupora utajiri na turathi ya nchi hizo.