OCHA: Yemen inakabiliwa na hali mbaya ya baa la njaa
(last modified Wed, 24 Oct 2018 07:52:37 GMT )
Oct 24, 2018 07:52 UTC
  • OCHA: Yemen inakabiliwa na hali mbaya ya baa la njaa

Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) imetangaza kuwa, nchi ya Yemen inakabiliwa na hali mbaya ya baa la njaa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana kujadili  hali ya kibinadamu nchini Yemen. 

Mark Lowcock amebainisha katika hotuba yake hiyo kwamba, baa la njaa linanyemelea Yemen na kwamba, takribani nusu ya watu wa Yemen hawana chakula cha kutosha. 

Mark Lowcock Mkuu wa Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA)

Mkuu wa Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) amekiambia kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, tahadhari aliyoitoa mwezi uliopita wa Septemba kuhusu uwezekano wa Yemen kukumbwa na baa la njaa inazidi kutimia kwani idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula katika nchi hiyo inazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Mkuu wa Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) anasema hayo katika hali ambayo, asasi mbalimbali za utoaji misaada ya kibinadamu zimeonya mara kadhaa kuhusiana na uhaba wa chakula nchini Yemen, nchi ambayo imeendelea kushuhudia mashambulio ya kijeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. 

Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zinaendelea kukosolewa kutokana na kutochukua hatua za maana kusitisha mashambulio hayo ya kijeshi dhidi ya nchi masikini ya Kiarabu.

Tags