Baba wa Tovuti ajuta, ataka kudhibitiwa chombo hicho
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49203-baba_wa_tovuti_ajuta_ataka_kudhibitiwa_chombo_hicho
Profesa wa Taasisi ya Teklonojia ya Massachusetts na mhadhiri katiika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Marekani, Tim Berners-Lee amesema kuwa amekatishwa tamaa na hali ya sasa ya mtandao wa Intaneti (Tovuti) baada ya kashfa kadhaa za jinsi taarifa za watu binafsi katika mitandao ya kijamii zinavyotumiwa vibaya kueneza chuki na uhasama.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 02, 2018 12:53 UTC
  • Baba wa Tovuti ajuta, ataka kudhibitiwa chombo hicho

Profesa wa Taasisi ya Teklonojia ya Massachusetts na mhadhiri katiika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Marekani, Tim Berners-Lee amesema kuwa amekatishwa tamaa na hali ya sasa ya mtandao wa Intaneti (Tovuti) baada ya kashfa kadhaa za jinsi taarifa za watu binafsi katika mitandao ya kijamii zinavyotumiwa vibaya kueneza chuki na uhasama.

Tim Berners-Lee ambaye alivumbu Tovuti mwaka 1989 amesema kuwa makampuni makubwa ya teknolojia yenye makao yake huko Silicon Valley, California kama Facebook na Google yamekuwa makubwa kupita kiasi na kuna haja ya kugawanywa iwapo hakutatoa makampuni ya upinzani yanayoweza kupunguza ushawishi wao.  

Berners-Lee amesema kashfa ya Cambridge Analytica ilikuwa suala muhimu sana lililobadilisha mitazamo yake kuhusiana na Tovuti na mitandao ya kijamii.

Baba wa Tovuti anaamini kuwa, hatua ya Mkurugenzi Mkuu na mmliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg kuwaomba radhi watumiaji wa mtandao huo wa kijamii kutokana na "kuvunja uaminifu" kwa weteja wake zaidi ya bilioni moja haitoshi kwa sababu mitandao hiyo ya kijamii ingali inatumiwa kueneza chuki.

Imebainika kuwa kampuni ya Uingereza Cambridge Analytica ilidukua taarifa binafsi za mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facbook kupitia programu maalumu ya utafiti uliofanywa na Aleksander Kogan na ambayo ilipakuliwa na mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo na kuchukua taarifa za watu wengine.

Machi mwaka huu Mkurugenzi Mkuu na mmliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg akiwaomba radhi watumiaji wa mtandao huo na kusema hicho ni kitendo cha uvunjifu wa uaminifu.

Mapema mwaka huu pia kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga alitishia kuwa, ataushtaki mtandao wa kijamii wa Facebook pamoja na kampuni ya Cambridge Analytica kwa kutumia jina lake katika kuendesha kampeni ya uchochezi na uhasama wa kikabila kwa ajili ya kuhujumu malengo yake ya kuwa Rais wa Kenya hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka jana 2017.

Raila Odinga

Vilevile Wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameulaumu mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuruhusu uchochezi wa machafuko na ukatili dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar.

Baba wa Tovuti, Tim Berners-Lee ndiye aliyebuni fikra hiyo ambayo awali ilipewa jina la "Meshi" na baadaye ikaja kujulikana kama Tovuti au World Wide Web.