Ufaransa yasisitiza kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49458-ufaransa_yasisitiza_kuheshimu_makubaliano_ya_nyuklia_ya_jcpoa
Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya Ulaya amesisitiza kuwa Paris inaheshimu na kufungamana na Makubaliano ya Nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji yaani JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 12, 2018 04:07 UTC
  • Ufaransa yasisitiza kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya Ulaya amesisitiza kuwa Paris inaheshimu na kufungamana na Makubaliano ya Nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji yaani JCPOA.

Akizungumza katika seneti ya nchi hiyo, Natalie Loizou ametoa radiamali yake kwa hatua ya Marekani ya kutekeleza duru ya pili ya vikwazo dhii ya Iran kuanzia tarehe 5 mwezi huu wa Novemba na kueleza kuwa: Mashirika ya Ufaransa yanatii na kufungamana na sheria na viwango vya Ulaya kwa msingi huo vikwazo vya Marekani dhidi ya mashirika hayo ni jambo lisilokubalika. 

Natalie Loizou ameongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti nyingi za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA), Iran imeheshimu na kufungamana na majukumu yake yote katika fremu ya makubaliano ya JCPOA na kwa sababu hiyo Ufaransa na waitifaki wake wa Ulaya na vile vile Russia na Uchina zimekuwa zikiyaunga mkono makubaliano hayo ya nyuklia.  

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe nane mwezi Mei mwaka huu alitangaza kwa upande mmoja kujitoa nchi yake katika makubaliano hayo ya nyuklia na akatangaza kurejeshwa vikwazo hivyo vya nyuklia dhidi ya Iran. Uingereza, Ufaransa, Russia, Uchina, Ujrumani na Umoja wa Ulaya zimepinga hatua hiyo ya Trump na kusisitiza kuyalinda makubaliano ya JCPOA na kuendelezwa uhusiano wa kibishara kati ya nchi hizo na Iran. 

Rais Donald Trump wa Marekani