Serikali ya Ufaransa yazidi kukandamiza raia wake + Video
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49906-serikali_ya_ufaransa_yazidi_kukandamiza_raia_wake_video
Polisi nchini Ufaransa wanaendelea kutumia nguvu kupita kiasi kukandamiza wananchi wanaopinga mfumo wa kibepari.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 02, 2018 04:32 UTC

Polisi nchini Ufaransa wanaendelea kutumia nguvu kupita kiasi kukandamiza wananchi wanaopinga mfumo wa kibepari.

Maandamano ya harakati ya wananchi maarufu kwa jina la "vijambakoti vya njano" yanaendelea huku jeshi la polisi na vikosi vya usalama vya nchi hiyo ya Ulaya vikiendelea kukandamiza raia kupita kiasi.

Machafuko yaliyoendelea hadi leo alfajiri baina ya wananchi na polisi huko Ufaransa yamepelekea makumi ya watu kujeruhiwa na kutiwa mbaroni. 

Jeshi la Ufaransa linatumia nguvu kupita kiasi kukandamiza maandamano ya wananchi

 

Mtandao wa habari wa RTE umeripoti kuwa, zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa na wengine wasiopungua 300 wametiwa mbaroni na polisi katika wiki ya tatu ya maandamano ya nchi nzima ya kulalamikia ughali wa maisha huko Ufaransa.

Mpango wa serikali ya Ufaransa wa kuongeza bei ya mafuta umezidi kupandisha juu gharama za maisha na kuwaweka kwenye hali ngumu wananchi wa nchi hiyo ya Ulaya. Ripoti zinasema kuwa hali mjini Paris ni mbaya sana hivi sasa.

Waandamanaji wanalalamikia siasa za Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wakisema kuwa zimewasababishia makali ya maisha ingawa hata hivyo Macron anaendelea kushikilia msimamo wake wa kutobadilisha siasa zake hizo.