Watu 1400 wakamatwa Ufaransa katika maandamano ya 'vizibao vya njano'
Watu zaidi ya 1400 wamekamatwa kote Ufaransa huku polisi na wanajeshi wakipamabana na waandamanaji wanaojulikana kama waandamanaji wa Vizibao vya Njano, ambao wanaendeleza malalamiko kuhusu ughali wa maisha.
Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machoezi na magari ya kijeshi ya deraya kuwadhbiti waandamanaji jana ambapo watu zaidi ya 135 walijeruhiwa na wengine wasiopungua 1,400 wamekamatwa.
Mji mkuu wa Ufaransa ulikuwa sawa na medani ya vita jana wakati wa mapigano makali baina ya maafisa wa usalama na waandamanaji waliokuwa na hasira.
Kwa ujumla karibu maafisa wa usalama, wakiwemo wanajeshi 89,000 wamesambazwa kote Ufaransa leo baada ya kuzuka wasiwasi kuwa waandamanaji, kama ilivyyokuwa Jumamosi iliyopita, mara hii pia watateketeza magari na kupora maduka.
Hii ni wikiendi ya nne ya maandamano ya Wafaransa dhidi ya ughali wa maisha na ongezeko la bei ya mafuta ya petroli. Waandamanaji wanataka Rais Emmanuel Macron aondoke madarakani kutokana na hali mbaya inayosuhudiwa nchini humo. Polisi Ufaransa wanatuhumiwa kukiuka haki za binadamu wakati wakikabiliana na waandamanaji wanaolalamika hali mbaya ya maisha.