Daily Mail: Polisi wa Ufaransa watatumia silaha ya kemikali kuzima maandamano
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50262-daily_mail_polisi_wa_ufaransa_watatumia_silaha_ya_kemikali_kuzima_maandamano
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limefichua kwamba yumkini polisi ya Ufaransa ikatumia silaha ya kemikali kwa ajili ya kuzima na kudhibiti maandamano na ghasia zinazoendelea katikati ya jiji la Paris.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 18, 2018 23:20 UTC
  • Daily Mail: Polisi wa Ufaransa watatumia silaha ya kemikali kuzima maandamano

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limefichua kwamba yumkini polisi ya Ufaransa ikatumia silaha ya kemikali kwa ajili ya kuzima na kudhibiti maandamano na ghasia zinazoendelea katikati ya jiji la Paris.

Ripoti iliyotolewa na gazeti hilo imesema kuwa, sambamba na maandamano yanayoendelea nchini Ufaransa kupinga sera za kiuchumi za serikali ya nchi hiyo na mfumo wa ubepari, kuna uwezekano polisi ya Ufaransa ikatumia poda ya kemikali inayodhoofisha waandamanaji kwa ajili ya kudhibiti harakati zao na kuwazuia kusonga mbele.

Gazeti hilo limeandika kuwa, hatua hiyo inayotazamiwa kuchukuliwa na vyombo vya usalama vya Ufaransa itakabiliwa na upinzani mkubwa wa jumuiya za kiraia na hata Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali.

Miji mbalimbali ya Ufaransa hususan Paris, imekuwa uwanja wa maandamano na ghasia kubwa baina ya vyombo vya usalama na waandamanaji wa harakati ya Vibao vya Njano wanaopinga sera za kiuchumi za Rais Emmanuel Macron.

Paris, Ufaransa

Watu wasiopungua 8 wameuawa hadi sasa katika machafuko hayo ya Ufaransa ambayo sasa yamepanuka na kuingia katika nyingine za Ulaya kama Uholanzi na Ubelgiji. Mamia ya waandamanaji wengine wamejeruhiwa na kutiwa nguvuni katika machafuko hayo ya Ufaransa yaliyoanza tarehe 17 Novemba.