Makasisi 700 wa Kanisa Katoliki Marekani watuhumiwa kulawiti watoto
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50303-makasisi_700_wa_kanisa_katoliki_marekani_watuhumiwa_kulawiti_watoto
Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Illinois nchini Marekani amewatuhumu makasisi 700 wa Kanisa Katoliki katika jimbo hilo kwamba wamewalawiti watoto, ikiwa ni idadi kubwa mno ikilinganishwa na ile iliyokuwa imetolewa na kanisa hilo huko nyuma.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 20, 2018 11:30 UTC
  • Makasisi 700 wa Kanisa Katoliki Marekani watuhumiwa kulawiti watoto

Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Illinois nchini Marekani amewatuhumu makasisi 700 wa Kanisa Katoliki katika jimbo hilo kwamba wamewalawiti watoto, ikiwa ni idadi kubwa mno ikilinganishwa na ile iliyokuwa imetolewa na kanisa hilo huko nyuma.

Katika taarifa, Lisa Madigan amesema Dayosisi ya Kanisa Katoliki katika jimbo hilo ilikiri kuwa makasisi na mapadri wake 185 tu ndio wamewalawiti watoto, huku ikificha kwa makusudi majina 500 ya viongozi wa kanisa hilo walioshiriki vitendo hivyo vya ufuska.

Mwanasheria Mkuu huyo wa Illinois amesema uchunguzi wao katika hatua zake za awali umebainisha kuwa, Kanisa Katoliki haliwezi kujiwajibisha na kujibebesha dhima ya vitendo viovu vinavyofanywa na viongozi wake.

Jimbo la Illinois lilianzisha uchunguzi huo baada ya ripoti ya uchunguzi katika jimbo jingine la Marekani la Pennsylvania kufichua kuwa, makasisi 300 wa kanisa hilo jimboni hapo waliwanajisi au kuwalawiti watoto zaidi ya elfu moja ndani ya miaka 70.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 

Haya yanajiri miezi michache baada ya maaskofu 31 wa kanisa hilo ambao ni raia wa Chile  kutangaza kujiuzulu wakiwa mjini Rome nchini Italia.

Kuna mamia ya kesi za ubakaji na ulawiti zinazowakabili makasisi wa kanisa hilo, ambazo zimerundikana katika mahakama za Ulaya na Marekani zikisubiri kufanyiwa uchunguzi, jambo ambalo limeshusha hadhi ya Kanisa Katoliki duniani.