Wimbi la kujiuzulu wafanyakazi wa serikali ya Marekani laongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51050-wimbi_la_kujiuzulu_wafanyakazi_wa_serikali_ya_marekani_laongezeka
Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuendelea kufunga shughuli za serikali ya Kuu na kuendelea kutowalipa mishahara wafanyakazi wake, imewafanya akthari ya wafanyakazi wa serikali hiyo kujiuzulu au kuomba kustaafu mapema.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 22, 2019 11:35 UTC
  • Wimbi la kujiuzulu wafanyakazi wa serikali ya Marekani laongezeka

Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuendelea kufunga shughuli za serikali ya Kuu na kuendelea kutowalipa mishahara wafanyakazi wake, imewafanya akthari ya wafanyakazi wa serikali hiyo kujiuzulu au kuomba kustaafu mapema.

Habari kutoka Marekani zinasema kwamba, wafanyakazi wengi wa serikali ya Marekani ambao kwa muda sasa hawajapokea mshahara kutokana na kuendelea kufungwa kwa shughuli za serikali, sasa wanajiuzulu au kuomba kustaafishwa mapema huku wengine wakifikia hatua ya kujiua. Televisheni ya Marekani CNN imeripoti kwamba, katika hali ambayo umepita mwezi mmoja sasa tokea hali hiyo ianze hivi sasa kumeibuka hofu kwa wafanyakazi wa serikali kujiuzulu wakiwemo wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini humo.

Wafanyakazi nchini Marekani wakiandamana

Hii ni kusema kuwa, sehemu ya serikali ya Marekani imesimama tangu tarehe 22 Disemba mwaka jana kutokana na kutofikiwa maridhiano kati ya Rais Donald Trump na baraza la Kongresi kuhusiana na bajeti ya ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico. Karibu wafanyakazi laki nane wa serikali hiyo wamelazimika kusalia majumbani kwao au kukosa mshahara kutokana na kuendelea kufungwa shughuli za serikali, suala ambalo katika wiki za hivi karibuni limepelekea kushuhudiwa maandamano ya wafanyakazi nchini humo.