Rais wa Ufaransa akosoa sera za Israel dhidi ya Wapalestina
-
Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema hatua ya Israel na kuzivamizi na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina imeweka hatarini mazungumzo baina ya utawala huo na Palestina.
Emmanuel Macron amesema katika hadhara ya waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin kwamba, kuendelea hatua kwa hatua uvamizi na kuzitwaa kwa mabavu ardhi za Palestina kunakofanywa na Israel kumeweka hatarini mazungumzo ya Tel Aviv na Wapalestina na hatua hiyo inazidisha machafuko na ukosefu wa amani.
Rais wa Ufaransa amesema Paris inahitilafiana na Tel Aviv katika masuala kama ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi na kuongeza kuwa, Ufaransa pia haiafikiani na Israel kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina kwa lengo la kutaka kubadilisha muundo wa jamii na jiografia ya maeneo hayo kwa maslahi ya Wazayuni.
Vilevile Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa akitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran kupitia hatua zinazoshabihiana zaidi na michezo ya kuigiza ambazo zimedhihakiwa na kuwa kichekesho katika vyombo vya habari.