Trump awatishia wanajeshi wanaomuunga mkono Maduro
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51651-trump_awatishia_wanajeshi_wanaomuunga_mkono_maduro
Rais wa Marekani amewatishia maafisa wa jeshi wa Venezuela wanaomuunga mkono Rais wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 19, 2019 04:12 UTC
  • Trump awatishia wanajeshi wanaomuunga mkono Maduro

Rais wa Marekani amewatishia maafisa wa jeshi wa Venezuela wanaomuunga mkono Rais wa nchi hiyo.

Rais Donald Trump jana alisema kuwa wanajeshi wa Venezuela ambao wanamuunga mkono Rais Nicolaus Maduro wa nchi hiyo wanauweka hatarini mustakbali na maisha yao. Trump aidha alisema kuwa machaguo yote yapo mezani katika hatua yake ya kuzidisha vitisho kwa serikali ya Venezuela.  

Rais halali wa Venezuela, Nicolaus Maduro 

Rais wa Marekani wakati huo huo amewatolea wito maafisa wa jeshi wa Venezuela kukubali msamaha wa wote uliopendekezwa na Juan Guaido kiongozi wa upinzani ambaye amejitangaza kuwa Rais wa Venezuela.  

John Bolton Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani pia ametoa matamshi ya uingiliaji katika masuala ya ndani ya serikali za sasa za Venezuela, Cuba na Nicaragua na kueleza kuwa usoshalisti umeyumbisha ulimwengu wa Magharibi. Aidha amedai kuwa Caracas ni sehemu ya kwanza wa pande tatu hizo ambayo imeporomoka kuanzia Januari mwaka huu. Juan Guaido Jumatano tarehe 23 Januari mwaka huu huku akiungwa mkono na Marekani na nchi waitifaki wake alijitangaza kuwa Rais wa Venezuela; hatua ambayo imetajwa na serikali na wananchi wa Venezuela kuwa ni mapinduzi dhidi ya Rais halali wa nchi hiyo Nicolaus Maduro.