Malalamiko ya Wademocrat wa Marekani kwa ripoti ya Mike Mueller
https://parstoday.ir/sw/news/world-i52422-malalamiko_ya_wademocrat_wa_marekani_kwa_ripoti_ya_mike_mueller
Ushindi wa ghafla na uliojaa utata alioupata Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwezi Novemba 2016 ulipokewa kwa hasira kubwa na chama cha Democrat cha nchi hiyo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 26, 2019 22:08 UTC
  • Malalamiko ya Wademocrat wa Marekani kwa ripoti ya Mike Mueller

Ushindi wa ghafla na uliojaa utata alioupata Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwezi Novemba 2016 ulipokewa kwa hasira kubwa na chama cha Democrat cha nchi hiyo.

Chama hicho kilisema kuwa Trump alisaidiwa na Russia kupata ushindi huo. Tuhuma hizo zilikuwa kubwa kiasi kwamba Marekani iliamua kuiwekea vikwazo Russia mwishoni mwa mwezi Disemba 2016 kwa madai ya kudukua na kutia mkono matokeo ya uchaguzi wa rais huko Marekani.

Tangu mwanzoni kabisa mwa urais wake, wapinzani wa Trump walikuwa na matumaini ya kupatikana ushahidi wa kuthibitha kwamba Warussia walivuruga matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Mike Mueller, alipewa jukumu la kufuatilia suala hilo na ripoti yake ilikuwa inasubiriwa kwa hamu ili kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani, iwezekane kupokonywa madaraka rais aliyepewa ushindi. Uchunguzi wa Mueller umechukua karibu miaka miwili na muda wote huo serikali ya Trump ilikuwa katika kibano na panda shuka nyingi. Katika kipindi hicho cha uchunguzi wake, Mueller ametuma maombi 2800, ametoa hukumu 500 za uchunguzi na amesaili mashahidi 500.

Donald Trump

 

Baada ya kupita muda mrefu wa kusubiri, hatimaye Mueller amekabidhi matokeo ya uchunguzi wake kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr. Naye Willam Barr alituma barua kwa Baraza la Congress na kusema kuwa, Mueller amewasilisha matokeo ya uchunguzi wake ambao unaonesha kuwa hakuna ushirikiano wowote uliokuwepo baina ya Trump na Russia wakati wa uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka 2016. Baada ya kutolewa tangazo hilo, Trump amejitokeza hadharani na kudai kuwa matokeo ya uchunguzi huo wa Mueller yanamvua na hatia na kwamba ataomba fidia kutoka kwa watu ambao walimtuhumu kushirikiana na Russia kupanga matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Hata hivyo wanachama wa chama cha Democrat ambao wana wingi wa viti katika Baraza la Congress hawakufurahishwa hata kidogo na matokeo ya uchunguzi huo na wametaka ripoti yote ya Mueller kuhusiana na suala hilo ioneshwe hadharani.

Ni jambo ililo wazi kwamba vitendo vilivyofanywa na Trump na wafuasi wake wakati uchunguzi wa Mueller ukiendelea, unamuweka rais huyo wa Marekani na wenzake katika hatari ya kufuatiliwa kisheria. Si hayo tu, lakini pia wawakilishi na maseneta wengi wa chama cha Democrat ambao wanataka ripoti ya Mueller itangazwe kikamilifu na isitangazwe kwa kufichwa-fichwa, bila ya shaka yoyote wataendelea kufuatilia kesi za huko nyuma za Trump na kuhakikisha rais huyo wa Marekani anaitwa kujieleza mbele ya Baraza la Congress. Bila ya shaka yoyote chama cha Democrats kinahitajia sana kupata kwa undani ripoti hiyo ya Müller kwa ajili ya kumpa ushindi mgombea wa chama hicho dhidi ya Trump katika uchaguzi wa mwaka 2020 huko Marekani. 

 

Tunapozingatia hayo tutaona kuwa, wanachama wa chama cha Democrats ambao wanapigania kuitwa Trump kujieleza, hawawezi kuliacha hivi hivi suala la kushirikiana Trump na Russia katika kupanga matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka 2016, na hapana shaka watataka kufuatiliwa vitendo vya rais huyo wa Marekani vilivyokuwa vinakwamisha uchunguzi wa suala hilo hasa kwa kuzingatia kuwa bado kuna maswali mengi ambayo hayamvui Trump na makosa kama vile kitendo cha mtoto wa kiume wa Trump kuonana na wakili wa Russia. Hadi hivi sasa haijulikani ni kwa nini mtoto huyo wa Trump alionana na kufanya mazungumzo na wakili huyo wa Russia.

Kiujumla ni kwamba Wademocrat huko Marekani wanaikosoa vikali  serikali ya Donald Trump. Kirsten Gillibrand seneta wa Marekani kutoka chama cha Democrat sambamba na kulaani mashambulizi ya Trump kwa thamani na taasisi za chama cha Democrat amesema kuwa, Trump anataka tuamini kwamba ana mabavu na nguvu wakati si kweli. Ukweli ni kwamba Trump ameangamiza muudo wa maadili wa Marekani.