Ufaransa yakosoa mpango wa 'Muamala wa Karne'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54047-ufaransa_yakosoa_mpango_wa_'muamala_wa_karne'
Licha ya juhudi kuibwa zinazofanywa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya kufanikisha mpango wa 'Muamala wa Karne' ambao unalenga kudhamini maslahi ya utawala haramu wa Israel kwa madhara ya Wapalestina, lakini washirika wa Ulaya wa Washington ikiwemo Ufaransa, wanaendelea kuukosoa mpango huo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 11, 2019 05:21 UTC
  • Ufaransa yakosoa mpango wa 'Muamala wa Karne'

Licha ya juhudi kuibwa zinazofanywa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya kufanikisha mpango wa 'Muamala wa Karne' ambao unalenga kudhamini maslahi ya utawala haramu wa Israel kwa madhara ya Wapalestina, lakini washirika wa Ulaya wa Washington ikiwemo Ufaransa, wanaendelea kuukosoa mpango huo.

Kuhusu hilo, Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa akiwa safarini nchini Morocco ameukosoa mpango huo wa 'Muamala wa Karne akisema kuwa hautakuwa na mchango wowote katika kuleta amani na utulivu katika eneo la Asia Magharibi. Amesema mtazamo wa Trump kuhusu utawala wa Israel na Wapalestina unaonyesha kuwa mpango wake huo hautaziridhisha pande zote mbili. Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesisitiza kuwa msimmao wa nchi hiyo ni kuwa hakuna mpango mwingine wowote utakaoweza kuleta amani kati ya pande mbili hizo isipokuwa kubuniwa kwa nchi mbili za Wapalestina na Waisreali na kuwawezesha kuishi pamoja kwa amani.

Ameashiria hatua ya upande mmoja ya Trump ya kuutambua rasmi mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel mwaka 2017 na kusema, Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya zingali zinaipinga hatua hiyo. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na wanachama 15 kati ya wanachama wote 16 wa Baraza la Usalama la umoja huo walipinga  hatua hiyo ya upande mmoja ya Washington. Mpango wa 'Muamala wa Karne unapingwa kimataifa kutokana na kutofautiana kwake na uamuzi pamoja na mpango mwingine wa amani uliowasilisha na pande za Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Russia na Marekani yenyewe.

Maandamano ya upinzani dhidi ya mpango wa 'Muamala wa Karne'

Akizungumzia suala hilo, Jean-Claude Juncker, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ameitaka Marekani izingatie na kutilia maanani kwa usawa mahitaji ya pande zote za Israel na Palestina inapowasilisha mpango wowote wa kuzipatanisha pande hizo. Jared Kushner, mkwe, mshauri na dalali wa Rais Trump kuhusiana na mpango wa 'Muamala wa Karne', alibainisha mtazamo wa rais huyo wa Marekani kuhusiana na masuala ya Asia Magharibi na hasa juhudi za kufanikisha mpango huo katika mazungumzo yake ya hivi karibuni na Junker pamoja na Fedirica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya. Baada ya kusikiliza maneno yake, umoja huo ulimfahamisha Kushner mtazamo wake, ambao unafanana na wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo.

Serikali ya Trump huko nyuma ilijaribu mara kadhaa kuuzindua mpango huo lakini ikalazimika kuuhairisha kutokana na sababu tofauti. Inasemekana mara hii pia huenda ikalazimika kuahirisha uzinduzi wake kutokana na kushindwa Benjamini Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel kuunda barala za mawaziri la utawala huo wa kibaguzi. Mpango huo hatari wa Trump na ambao una madhara makubwa kwa Wapalestina na Waislamu wote kwa ujumla, unauchukulia mji mtakatifu wa Quds kuwa mali na mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, unaupa sehemu kubwa ya Ukongo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwapokonya wakimbizi wa Kipalestina haki yao ya msingi ya kurejekea katika ardhi zao za asili ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu. Jambo hilo limeipelekea hata Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambayo hadi sasa imelegeza msimamo na kutoa fursa nyingi kwa utawala huo, kupinga vikali mpango huo wa Trump wa eti 'Muamala wa Karne'. Mamlaka hiyo ya utawala wa ndani imesimamisha mazungumzo yote na Marekani tokea Trump alipochukua uamuzi wa kuuhamishia ubalozi wake huko Quds kutoka mjini Tel Aviv mwaka uliopita, kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wasaudia, wasaliti wakubwa wa malengo ya Palestina

Hivi sasa serikali ya Trump imechukua uamuzi wa kutekeleza hatua ya kwanza ya mpango wa 'Muamala wa Karne' kupitia kongamano ambalo imeliandaa huko Manama, mji mkuu wa Bahrain ili ipate kuchangisha pesa za utekelezaji wake kutoka kwa nchi na mashirika yatakayoshiriki kongamno hilo. Krushner na Jason Greenblatt, mwakilsihi wa Marekani katika Masuala ya Asia Magharibi wamepewa jukumu la kuendesha kongamano hilo. Marekani kwa sasa inatoa mashinikizo makubwa dhidi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu ili zipate kushiriki kongamano hilo la hiana. Siku chache zilizopita, Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema kuwa, anataraji kwamba nchi za Kiarabu zitashiriki kongamano hilo ili kwa uchache zipate kusikia yatakayosemwa humo. Alisema hakuwa na matumaini makubya ya nchi hizo kutekeleza wala kutetea yale yote yatakayofikiwa katika kongamano hilo.