Umoja wa Mataifa wakiri kutotilia maanani suala la wakimbizi wa Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54203-umoja_wa_mataifa_wakiri_kutotilia_maanani_suala_la_wakimbizi_wa_myanmar
Umoja wa Mataifa umekiri kupitia ripoti yake kuhusu kutokuwa na natija utendaji wa taasisi hiyo ya kimataifa mkabala wa wakimbizi wa Myanmar.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 18, 2019 13:33 UTC
  • Umoja wa Mataifa wakiri kutotilia maanani suala la wakimbizi wa Myanmar

Umoja wa Mataifa umekiri kupitia ripoti yake kuhusu kutokuwa na natija utendaji wa taasisi hiyo ya kimataifa mkabala wa wakimbizi wa Myanmar.

Baada ya Umoja wa Mataifa kutuhumiwa kupuuza kuongezeka mashambulizi na utumiwaji mabavu huko Myanmar dhidi ya wakimbizi; Antonio Guterres Katibu Mkuu wa umoja huo ameagiza kuchunguzwa utendaji wa taasisi hiyo ya kimataifa kuhusiana na wakimbizi wa Myanmar. Ripoti kuhusu utendaji kazi wa  Umoja wa Mataifa imetayarishwa na Gert Risenthal Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Guatemala; na inaonyesha kuwa utendaji wa umoja huo umesababisha Waislamu wa kabila la Rohingya kuwa wakimbizi mwaka juzi wa 2017. 

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 

Jeshi la Myanmar mwezi Agosti mwaka juzi lilitekeleza mashambulizi na ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa jamii hiyo ya waliowachache katika jimbo la Rakhine magharibi mwa nchi hiyo; hatua iliyotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni maangamizi ya kizazi. Hivi sasa zaidi ya wakimbizi laki saba wa Rohingya wamekimbilia Bangladesh baada ya kuvuka mpaka wa Myanmar.