Trump asema uongo mara 27 katika hotuba ya dakika 95
Televisheni ya CNN imeripoti kuwa Rais wa nchi hiyo ametoa madai ya uongo mara 27 kupitoa hotuba yake iliyochukua muda wa dakika 95.
Televisheni ya CNN imechunguza matamshi hayo ya uongo ya Rais Donald Trump wa Marekani na kueleza kuwa, Trump Jumatatu usiku wiki hii alitoa hotuba katika mikutano yake ya uchaguzi huko New Mexico kwa muda wa dakika 95 na kutoa madai ya uongo yasiyopungua 27; ambapo aghalabu ya madai hayo ya urongo alishawahi kuyatoa hadharani miezi kadhaa iliyopita.
Kwa mfano, Trump alisema kuwa, miaka 15 iliyopita Venezuela ilikuwa moja ya nchi tajiri sana duniani katika hali ambayo nchi hiyo ya Amerika ya Latini mwaka 2004 ilishika nafasi ya 67 kati ya nchi tajiri duniani. Televsiheni ya CNN imeripoti kuwa, Rais wa Marekani aidha alisema kuwa Wademocrat wanataka mipaka iwe wazi na kwamba uchumi wa China pia katika kipindi cha miaka 57 iliyopita ulikuwa katika hali mbaya sana; matamshi ambayo yote ni ya uwongo.
Takwimu na chunguzi mbalimbali za maoni zinaonyesha kuwa, Donald Trump amezidi kupoteza hali ya kuaminiwa siku baada ya siku kwa sababu mwaka juzi wa 2017 alitoa matamshi ya uongo 24.9 hata hivyo kuanzia mwaka jana hadi mwezi Mei mwaka huu Trump kwa siku amekuwa akitoa madai 8.3 ya uongo.