Democrats wataka Marekani iikatie Israel misaada ya kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57012-democrats_wataka_marekani_iikatie_israel_misaada_ya_kijeshi
Wagombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani wamesema serikali ya Washington inapaswa kusitisha misaada ya kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, iwapo utaendelea kupora na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2019 09:01 UTC
  • Democrats wataka Marekani iikatie Israel misaada ya kijeshi

Wagombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani wamesema serikali ya Washington inapaswa kusitisha misaada ya kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, iwapo utaendelea kupora na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Seneta Bernie Sanders kutoka chama cha Democrat alisema jana Ijumaa katika mkutano wa hadhara kuwa, "Dola bilioni 3.8 ni nyingi mno. Sehemu ya fedha hizo inapaswa kuelekezwa mara moja kama msaada wa kibinadamu huko Gaza."

Marekani huupa utawala wa Kizayuni wa Israel dola bilioni 3.8 kama msaada wa kijeshi kila mwaka.

Huko nyuma pia, Seneta huyo mashuhuri wa Marekani ambaye kiasili ni Myahudi aliukosoa vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kufuata amri ya Donald Trump ya kuwazuia wabunge wawili Waislamu wa Marekani kuingia Quds tukufu. 

Seneta Elizabeth Warren, mwanasiasa mwingine mkosoaji mkubwa wa Trump na Israel

Wabunge Ilhan Omar na Rashida Tlaib ambao ni Waislamu wa kwanza wa kike kuchaguliwa katika Kongresi ya Marekani na walitarajiwa hivi karibuni kufanya safari katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na vilevile kuzuru Msikiti wa al Aqsa.

Wagombea wengine wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani, Seneta Elizabeth Warren na Pete Buttigieg, Meya wa South Bend, Indiana wamekuwa wakitumia majukwaa ya mikutano yao ya kampeni kukosoa vikali sera ghalati za utawala haramu wa Israel na hata hata kukosoa misimamo ya kuchupa mipaka ya Trump.