Wademocrat wajiandaa kususia hotuba ya kila mwaka ya Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i58923-wademocrat_wajiandaa_kususia_hotuba_ya_kila_mwaka_ya_trump
Wabunge wa chama cha Democrat katika bunge la wawakilishi nchini Marekani, sambamba na kufanya harakati za malalamiko, wanajiandaa kususia hotuba ya kila mwaka ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2020 10:14 UTC
  • Wademocrat wajiandaa kususia hotuba ya kila mwaka ya Trump

Wabunge wa chama cha Democrat katika bunge la wawakilishi nchini Marekani, sambamba na kufanya harakati za malalamiko, wanajiandaa kususia hotuba ya kila mwaka ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Sambamba na kukaribia hotuba ya kila mwaka ya rais huyo ambayo itajiri kesho Jumanne, wanawake wa chama cha Democrat nchini Marekani wanaandaa harakati ya malalamiko kama ile iliyofanyika pia mwaka jana kwa kuvalia nguo nyeupe kwa lengo la kuonyesha mshimakamano wao na wanawake wengine. Katika uwanja huo Steve Cohen, mbunge wa chama cha Democrat amesema kuwa, hayupo tayari kwenda kwenye kikao hicho na kusikiliza maneno ya uongo ya Trump.

Trump na matatizo yanayomkabili

Naye Al Green mbunge wa Democrat wa jimbo la Texas na ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wanaounga mkono mpango wa kumsaili rais huyo na ambaye kwa muda wote amekuwa akisusia hotuba zote za Trump hadi leo, amesema kuwa msimamo wake bado haujabadilika kuhusiana na suala hilo. Kwa akali wabunge 6 wa chama hicho tayari wametangaza kususia hotuba ya kila mwaka ya Trump. Mwaka 2018 wabunge 14 wa chama hicho pia walisusia hotuba ya kila mwaka ya rais huyo katika bunge la wawakilishi. Katika hotuba ya kesho Trump atakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu Disemba 2019 na Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi, baada ya kupasishwa mpango wa kusailiwa kwake kufuatia sakata la kashfa ya Ukraingate.