Mar 10, 2020 02:46 UTC
  • Indhari yatolewa juu ya uwezekano wa kuendelea kujiua askari wa Marekani

Matokeo ya uchunguzi mpya yanaonyesha kwamba, karibu nusu ya askari wa Marekani hufikirla kujiua baada ya kujiunga na jeshi.

Matokeo hayo ya uchunguzi mpya uliopewa jina la 'Askari Wakongwe wa Vita vya Afghanistan na Iraq' yanaonyesha kwamba asilimia 44 ya askari wa Marekani huwa na fikra ya kujiua tangu wanapojiunga na jeshi la nchi hiyo. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kila mmoja kati ya theluthi mbili ya watu waliosailiwa amesema, kwa uchache anamjua askari aliyejiua nchini humo katika vita vya baada ya Septemba 11, 2001.

Askari wakongwe wa Marekani walioshiriki vita vya Iraq na wanaharakati wanaopinga vita nchini humo wamesema kuwa takwimu hizo si za kushangaza na wamekuwa wakitahadharisha kuhusu ongezeko la mwenendo wa kujiua askari wakongwe wa nchi hiyo.

Idadi ya askari wa Marekani wanaojiua inatisha sana

Viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) wanadai kuwa, akthari ya askari wanaojiua wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia. Mwezi Novemba mwaka jana pia gazeti la New York Times liliandika kuwa, zaidi ya askari wakongwe elfu 45 wa Marekani au askari waliohudumu ndani ya jeshi hilo kwa miaka sita, walijiua.

Gazeti hilo limeandika kuwa, askari 20 wa Marekani hujiua wenyewe siku, suala ambalo linaonyesha kuwa idadi ya askari wanaopoteza maisha kwa njia hiyo ni zaidi ya askari wote waliouawa katika vita vya Afghanistan na Iraq.

Tags